Achana na kiwango bora anachoonyesha kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika, Clatous Chama ni lulu katika kikosi cha Simba
Ndani ya ligi kuu ya Vodacom, Chama ndiye mchezaji mwenye athari zaidi kwa timu pinzani
Amehusika katika mabao 17 kati ya mabao 51 yaliyofungwa na Simba msimu huu
Mguu wake umeweka kambani mabao saba na kutengeneza mabao mengine 10
Ndiye kinara wa kutengeneza mabao akifuatiwa kwa karibu na Luis Miquissone ambaye naye akiwa na pasi 9 za mabao
Ligi ya Tanzania imempenda Chama na hakika anaitendea haki. Huu ni msimu wake wa nne ndani ya klabu ya Simba
Hakika ni wakati bora sana kwake kuwa mchezaji wa Simba
ADVERTISE HERE