Tuko tayari kumkabili yeyote ligi ya mabingwa - Gomes

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
15 Apr 2021
Tuko tayari kumkabili yeyote ligi ya mabingwa - Gomes

Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes amesema kuwa amewaambia wachezaji wake wanapaswa kuonyesha ukubwa walionao kwa kupata matokeo chanya kwenye mechi zote za ligi pamoja na zile za kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika

Tayari Simba imetinga hatua ya robo fainali ikiwa inaongoza kundi A na pointi 13 inafuatiwa na vigogo Al Ahly ambao wana pointi 11 wakiwa nafasi ya pili.

Aprili 30 inatarajiwa kuchezwa droo ya michuano hiyo mikubwa. Gomes amesema kuwa anasubiri kuona wapinzani atakaopangiwa kucheza nao huku akibainisha kuwa wote anawatambua kutokana na kuwa na data zao pamoja na uzoefu wa soka la Afrika.

"Ukizungumza kuhusu Simba kwa sasa ni moja ya timu kubwa Afrika, hivyo nimewaambia wachezaji kwamba lazima waonyeshe ukubwa wao kwenye mechi zote ambazo tutacheza iwe ni kwenye ligi ama robo fainali.

"Kwa wakati huu tunawekeza nguvu zetu kwenye mechi za ligi ila haina maana kwamba tutapuuzia kuhusu mechi zetu za robo fainali kwani hiyo nayo ni mipango yetu kuona kwamba tunafanya vizuri.

"Natambua soka la Afrika vizuri na changamoto zake, nimefundisha Algeria ninazitambua timu za huko namna ilivyo na Afrika Kusini pia nina marafiki na data zao ninazo hivyo hakuna haja ya kuwa na hofu katika hilo," amesema

Timu ambazo zinaweza kukutana na Simba kwenye hatua ya robo fainali ni pamoja na CR Belouizdad ipo nafasi ya 10 na pointi 26 baada ya kucheza mechi 15 na MC Alger ipo nafasi ya 11 na pointi 25 baada ya kucheza mechi 16 hizi ni za Algeria na Kaizer Chiefs ni ya Afrika Kusini ipo nafasi ya 9 na pointi 24 baada ya kucheza mechi 20

GPL

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’