Baada ya kuishushia Mtibwa Sugar kipigo cha mabao 5-0 hapo jana, Simba inatarajiwa kuelekea mkoani Shinyanga ambako April 18 wanakabiliwa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Mwadui Fc
Mabingwa hao wa nchi watakuwa na michezo mitatu kanda ya ziwa kabla ya kurejea jijini Dar es salaam kuivaa Dodoma Jiji April 27
April 21 watacheza na Kagera Sugar mkoani Kagera kisha kuelekea Misungwi kuifuata Gwambina Fc April 24
Simba itakuwa na uhakika wa kurudi kileleni mwa msimamo wa ligi pale mechi hizi zitakapokuwa zimemalizika
Mpaka sasa Simba inashika nafasi ya pili ikiwa imekusanya alama 49, alama mbili nyuma ya Yanga yenye alama 51
Simba ina michezo mitatu ya viporo
ADVERTISE HERE