Kiung Simba Sc Gersono wa zamani wa klabu ya Simba Gerson Fraga Vieira amesema kuwa amepona majeraha yake ya muda mrefu na hivyo atarejea uwanja
Fraga ameweka wazi kuwa anatamani kurejea katika klabu ya Simba katika usajili wa msimu ujao
Fraga aliachwa na Simba wakati wa dirisha dogo kutokana na majeraha ya goti aliyoyapata kwenye mechi dhidi ya Biashara United ambayo yamemfanya akae nje kwa zaidi ya miezi sita
Nyota huyo wa zamani wa timu ya Taifa ya vijana ya Brazil, baada ya kuuguza majeraha kwa takribani miezi saba, amewahakikishia mashabiki wa Simba kuwa yuko fiti na yupo tayari kurudi kwenye timu hiyo ambayo inatamba katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika
ADVERTISE HERE