Kupitia ukurawa wake wa mtandao wa Instagram, Mkuu wa Kitengo cha Habari na Mawasiliano klabu ya Simba, Haji Manara amewapa kongole kiungo Shiza Kichuya na washambuliaji John Bocco na Emanuel Okwi kwa mafanikio waliyoipa Simba mpaka sasa msimu huu.
Haijaandikwa na kusemwa kokote..najua hujui ngoja nikujuze.., ameandika Manara
Okwi, Bocco na Kichuya kwa pamoja wamefunga magoli 38 kati ya magoli 52 ya Simba kwenye michezo 22 ya mashindano rasmi waliyocheza Simba hadi sasa.
Mashindano rasmi waliyocheza ni pamoja na Ligi kuu,kombe la Shirikisho CAF na Kombe la Shirikisho la Azam.
Ukiachana na magoli hayo ambayo ni sawa na 73%ya magoli yote ya Simba 52, wachezaji hao kwa pamoja wameassist magoli 33.
Ndio combination bora kuwahi kutokea kwenye VPL ktk kipindi cha miaka kumi nyuma..iite KIBO..Kichuya.Boko na Okwi.....rudia tena KIBO
Simba iko kileleni mwa msimamo wa ligi kuu ya Vodacom ikiwa imejikusanyia alama 45, alama nane zaidi ya Yanga iliyo nafasi ya pili.
Okwi ndiye kinara wa mabao akiwa amefunga mabao 16 huku John Bocco akiwa nafasi ya tatu na mabao yake 10.
Shiza Kichuya aliyebadilishiwa majukumu na benchi jipya la ufundi, ana mabao saba.

ADVERTISE HERE