Kocha Msaidizi wa Simba, Seleiman Matola, amekiri kuwa Mtibwa Sugar imekuwa ikiwasumbua lakini safari hii wamejipanga kukabiliana nao ili kuibuka na ushindi kesho.
Akizungumzia maandalizi ya mchezo huo wa Ligi Kuu Tanzania utakaochezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam, Matola amesema kwa sasa nguvu zao wanaelekeza Ligi Kuu."
"Mchezo wetu wa kesho dhidi ya Mtibwa Sugar utakuwa mgumu kwa kuwa tunacheza na timu inayotusumbua mara nyingi, ila tumejiandaa
"Tumetimiza kile tulichokihitaji Kimataifa, nguvu zetu sasa tunaelekeza Ligi Kuu kwa sababu huwezi kushiriki Ligi ya Mabingwa bila kufanya vizuri Ligi Kuu," amesema Matola
Nae nahodha msaidizi wa Simba Mohammed Husein, amesema wamejipanga kuhakikisha wanashinda mechi zao ili waweze kutetea ubingwa bila ya kujali matokeo ya wapinzani wao
"Lengo letu ni kutetea ubingwa, tumejipanga kuhakikisha tunashinda kila mchezo bila kuangalia wapinzani wetu wanafanya nini," amesema