Beki tegemeo wa Simba na timu ya Taifa ya Kenya Joash Onyango amesema wachezaji wote wamefarijika kuona wamefanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika wakiwa vinara wa kundi A
Onyango amesema kwa sasa mawazo yote ni kuona wanaweza kutinga nusu fainali ya michuano hiyo mikubwa kabisa barani Afrika kwa ngazi ya vilabu
Licha ya kufungwa katika mchezo wa mwisho wa makundi dhidi ya Al Ahly, Simba imeongoza kundi A ikijikusanyia alama 13, ambazo ni alama mbili zaidi ya Al Ahly mabingwa watetezi ambao wamemaliza katika nafasi ya pili
"Haikuwa kazi rahisi lakini tunashukuru kufika hatua ya robo fainali. Ila kwa sasa lengo letu kuu ni kufika nusu fainali. Ni wazi ushindani utaongezeka katika hatua tuliyofika lakini nasi hatukufika hapa kwa bahati mbaya
"Tutaendelea kupambana kusaka matokeo ndani ya uwanja ili tufanikishe lengo letu lakini pia kuwapa furaha mashabiki wetu ambao wanatuunga mkono kwa bidii wakati wote,"Β alisema Onyango
Droo hatua ya robo fainali itapigwa April 30 Simba ikitarajiwa kupangwa na kati ya Kaizer Chiefs (Afrika Kusini), MC Alger (Algeria) na CR Belouizdad (Algeria)