Mwaka 2005 kocha msaidizi wa Simba Selemani Matola wakati huo akiwa kiungo mahiri na nahodha wa mabingwa hao wa nchi alipata nafasi kwenda kusakata kabumbu nje ya nchi kule Afrika Kusini
Matola alisajiliwa na klabu ya Super Sport United ambayo aliitumikia kwa misimu miwili
Kocha huyo Msaidizi wa timu ya Taifa, amefichua kuwa wakati akiitumikia Super Sport United, aliyekuwa kocha wao ni Pitso Masemane ambaye kwa sasa anainoa timu ya Al Ahly
Wawili hao walikutana katika mechi mbili zilizokutanisha Simba na Al Ahly na kila timu kushinda mechi ya nyumbani
Wakati akiwa mchezaji, Matola alipita katika mikono ya makocha mahiri
Haishangazi kuona nae anapita katika mkondo uleule
ADVERTISE HERE