Baada ya Simba kuipiga mkono Mbao FC, Stand United wajiandae kisaikolojia

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 Feb 2018
Baada ya Simba kuipiga mkono Mbao FC, Stand United wajiandae kisaikolojia
Baada ya ushindi mnono wa mabao 5-0 dhidi ya Mbao FC juzi, Simba inashuka tena dimba la Taifa keshokutwa Ijumaa kuivaa Stand United kwenye mchezo mwingine wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 20.

Mchezo huo ambao awali ulipangwa kupigwa Jumapili, March 04 ulirudishwa March 02 ili kuipa nafasi Simba kujiandaa na mchezo wa kombe la shirikisho mzunguuko wa kwanza dhidi ya Al Masry unaopigwa March 07.

Kocha Msaidizi wa Simba Masudi Djuma amesisitiza kuwa watahakikisha kikosi chao kinaibuka na ushindi ili kuendelea kuwa kileleni kwa tofauti ya alama nyingi dhidi ya wapinzani wao.

Naye beki mahiri wa kushoto Asante Kwasi amesema licha ya ushindi mnono walioupata dhidi ya Mbao FC hauwafanyi waidharau Stand United watakaocheza nao, Ijumaa ya hii kwenye Uwanja wa Taifa.

Kwasi alisema ligi ni ngumu na matokea hayatabiri, hilo ndilo jambo linalowafanya wawe na nidhamu na kila mchezo ili wasije wakatoka kwenye malengo ya kuwania taji la ubingwa.

"Nidhamu ni kitu pekee, kitakacholeta mapinduzi ndani ya klabu hiyo yenye hamu ya kutwaa ubingwa wa ligi baada ya Yanga, kuchukua mara tatu mfululizo."

"Mashabiki wanatusifia pale tunapofanya kazi nzuri, ikitokea tukachemka hakuna urafiki, ndio maana nasema kuwafunga Mbao jana mabao 5-0, hakumanishi tumafika mwisho hapana inatokea na ndio mpira ulivyo kote duniani," alisema.

Tayari uongozi wa Simba umetoa taarifa kuwa mshambuliaji wake Enmanuel Okwi aliyepata majaraha kwenye mchezo dhidi ya Mbao FC atakuwa fiti kuivaa Stand United.

Bado nahodha John Bocco anaendelea na matibabu ya kifundo cha mguu na huenda asiwe tayari kuivaa Stand United lakini upo uwezekano mkubwa atakuwepo kwenye mchezo dhidi ya Al MAsry March 07.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
9h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
15h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
18h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
21h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
21h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
22h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’