Gomes apania kuendeleza dozi za ligi ya mabingwa VPL

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
12 Apr 2021
Gomes apania kuendeleza dozi za ligi ya mabingwa VPL

Mabingwa wa nchi Simba keshokutwa Jumatano watashuka kwenye uwanja wa Benjamin Mkapa kuikaribisha Mtibwa Sugar katika mwendelezo wa ligi kuu ya Vodacom

Mchezo huo utapigwa kuanzia saa moja kamili usiku

Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema wanarejea kwenye ligi kwa lengo moja tu, kuhakikisha wanafanikisha mpango wa kutetea ubingwa

Gomes amesisitiza kuwa Simba haitapuuza michuano yoyote, lengo kuu ni kushinda ubingwa wa ligi kuu pamoja na FA huku pia wakiwa na nafasi ya kufanya makubwa zaidi kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika ambayo wako hatua ya robo fainali

"Tunahitaji kufanya vizuri katika kila shindano, tumetinga hatua ya robo fainali katika Ligi ya Mabingwa Afrika, lakini bado tuna jukumu la lufanya vizuri kwenye Kombe la FA na Ligi Kuu ya Tanzania, hayo ndio malengo yetu," amesema Gomes

Aliongeza morali waliyonayo wachezaji wake kupitia michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika, inampa matumaini ya kuendelea kupata matokeo chanya katika michezo itakayofuata.

"Hatutajamaliza kazi, bado msimu haujamalizika, naweza kusema safari inaelekea mwisho lakini hatujaimaliza, tunahitaji kuendelea kujituma ili tufikie malengo ya kila mmoja wetu" 

Baada ya mchezo dhidi ya Mtibwa Sugar Jumatano, Simba itasafiri kwenda Shinyanga kuwafuata Mwadui FC katika mechi itakayochezwa Aprili 18, mwaka huu na siku tatu baadaye itakuwa Bukoba kuwavaa wenyeji Kagera Sugar na Aprili 24, mwaka huu itawafuata Gwambina FC

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
24m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’