Michezo ya hatua ya makundi michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika imekamilika hapo jana na timu zote zilizofuzu makundi kupatikana
Kundi A Simba imetinga robo fainali ikiwa vinara wa kundi Al Ahly ya Misri wakiingia wakiwa washindi wa pili
Kundi B Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini ndiye mshindi wa kwanza akifuatiwa na CR Belouizdad ya Algeria iliyoshika nafasi ya pili
Kundi C Wydad Athletic ya Algeria imeongoza kundi wakati mshindi wa pili ni Kaizer Chiefs ya Afrika Kusini
Kundi D Esperance ya Tunisia imeongoza wakati MC Alger kutoka Algeria imeshinda nafasi ya pili
Timu moja kati ya CR Belouizdad, Kaizer Chiefs au MC Alger itachuana na Simba hatua ya robo fainali Simba ikitarajiwa kuanzia ugenini
Droo ya robo fainali itafanyika April 30
ADVERTISE HERE