Djuma 'afagilia' mziki wa Simba

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
28 Feb 2018
Djuma 'afagilia' mziki wa Simba
Huku ikiwa inaongoza ligi kwa kuwa na pointi 45 na mabao 46, Simba imezichimba mkwara klabu za ligi kuu na kuzitahadharisha juu ya kasi ya mshambuliaji wao Emmenuel Okwi.

Vinara hao wa ligi juzi walilitoa kipigo cha nguvu cha mabao 5-0 kwa Mbao FC kwenye mchezo uliochezwa Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Kocha msaidizi wa Simba, Masoud Djuma, alisema kuwa kasi waliyonayo sasa haichagui aina ya timu bali wamejipanga kutembeza vipigo kwa timu yoyote.

"Kwetu kazi ndio imeanza, kila mchezo sasa hivi ni kama fainali kwetu..., hatuangalii ni timu gani tunatecheza nayo, kikubwa tunataka kufikia malengo yetu," alisema Djuma.

Alisema kuwa kocha mkuu hiyo, Pierre Lechantre, ametoa majukumu kwa kila mchezaji na matokeo wanayoyapata yanatokana na wachezaji hao kutimiza majukumu yao.

"Unaona mashabiki walikuwa wanapiga kelele kuwa Kichuya (Shiza) afungi na kama vile amepunguza kasi, hapana, kuna majukumu amepewa, kazi yake si kufunga," alisema Djuma.

Aidha, Djuma, alisema kuwa kasi ya mshambuliaji wake, Emmanuel Okwi, wapinzani wao wajipange kumzuia.

"Okwi ni mshambuliaji aliyekamilika, ana akili ya mpira na mabeki wanatakiwa kutumia akili kumzuia.., unaona namna alivyocheza na Mbao," alisema.

Mabao mawili aliyofunga kwenye mchezo wa juzi dhidi ya Mbao FC yamemfanya Okwi, kumfunika mfungaji bora wa ligi msimu uliopita, Simon Msuva, ambaye alifunga mabao 14 kwa msimu wote akiwa na Yanga kabla ya msimu huu kujiunga na klabu ya Diffa al Jadida.

Okwi amefikisha idadi ya mabao 16 kutokana na michezo 19 tu huku akiwa na nafasi ya kuongeza kutokana na kubaki michezo 11 kabla ya kumalizika kwa ligi kuu msimu huu.

Mchezo unaofuata Simba itaumana na Stand United kwenye uwanja wa Taifa keshokutwa Ijumaa.
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
9h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
12h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
13h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
15h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
19h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’