Licha ya kujumuishwa katika kikosi kilichosafiri nchini Misri kwa ajili ya mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Al Ahly ambao utapigwa saa nne usiku wa leo Ijumaa, winga Bernard Morrison atakosa mchezo huo akitumikia adhabu ya kadi mbili za njano
Morrison alipewa kadi za njano katika michezo iliyopita dhidi ya Al Merrikh na AS Vita na kulingana na kanuni za CAF, mchezaji anapokuwa na kadi mbili za njano, anakosa mchezo mmoja
Hata hivyo licha ya mchango wake mkubwa katika michezo iliyopita, kukosekana kwake haliwezi kuwa tatizo kwani wapo wachezaji wa kuziba nafasi yake
Lakini pia Simba itacheza mchezo huo bila ya kuwa na presha yoyote ya matokeo kwani tayari wameshatinga robo fainali wakijihakikishia kumaliza vinara wa kundi A
Matokeo ya mchezo wa leo hayatabadili chochote katika msimamo wa kundi A