Mabingwa wa nchi Simba wako kule Misri kuendelea na majukumu ya Kimataifa ambapo leo majira ya saa nne usiku watakuwa na mchezo wa kukamilisha ratiba dhidi ya Al Ahly katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Baada ya kujihakikishia kutinga robo fainali na kumaliza hatua ya makundi wakiwa kileleni, kikosi cha Kocha Didier Gomes leo kitakuwa na kazi moja tu, kulinda heshima
Gomes amesema hawakwenda Misri kutalii bali wamepania kumaliza mechi zote za makundi bila ya kupoteza mchezo
Kocha huyo raia wa Ufaransa amesema kikosi chake kiko kamili, hakuna majeruhi, wako tayari kuwakabili mabingwa hao watetezi michuano ya ligi ya mabingwa
Nae mshambuliaji Meddie Kagere 'MK14' amesema watahakikisha wanawapa furaha mashabiki wao huku nyumbani ambao siku zote wanaamini wao ni washindi
Kila la kheri Simba, kila la kheri wababe wa soka ukanda wa Afrika Mashariki na kati