Wakati mabingwa wa nchi Simba wakiwa kule Misri ambako kesho Ijumaa watashuka dimbani kuwakabili Al Ahly katika mchezo wa kukamilisha ratiba ligi ya mabingwa barani Afrika, Mtendaji Mkuu Barbara Gonzalez amesema Al Ahly ni timu iliyokamilika ndani na nje ya uwanja na kuwa yapo mambo ambayo Simba wanaweza kunufaika kutoka kwa timu hiyo
Kabla ya michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu, Barbara alipata nafasi ya kuitembelea Al Ahly kujionea namna klabu hiyo inavyoendeshwa
Al Ahly ndio klabu kongwe na yenye mafanikio zaidi barani Afrika
Klabu hiyo inatajwa kuwa na makombe mengi zaidi duniani. Lakini pia inaamiwa kuwa ndio klabu tajiri zaidi barani Afrika
Simba pia iko katika mwelekeo huo, msimu huu ikidhihirisha kuwa iko tayari kwenda sawa na miamba hao wa soka barani Afrika ikifanikiwa kumaliza hatua ya makundi juu yao
"Kiuhalisia timu ya Al Ahly inabaki kuwa alama kwa timu za mpira wa miguu barani Afrika. Hii inakwenda mbali zaidi hadi nje ya uwanja. Kutokana na hayo tunapaswa kuhamasika na vitu kama"
(i) Uwezeshaji na miundombinu
(ii) Kiuchumi na miundo na mifumo ya utendaji na uendeshaji
(iii)Tathmini ya wachezaji (na mali nyingine)
(iv) Uchambuzi wa mitandao wa kijamii
(v) Utendaji wa kimichezo
Ni sehemu ya ujumbe wa Barbara alioweka katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii