Afisa Habari wa Mtibwa Sugar Thobias Kifaru ameipongeza Simba kwa kutinga hatua ya Robo Fainali ya Ligi ya Mabingwa Afrika na kusema klabu hiyo imemfurahisha.
Kifaru amesema Simba imemfurahisha si kwa sababu ni shabiki wake lakini hatua hii na namna ambavyo inazungumzwa Tanzania Afrika nzima.
"Niwapongeze wachezaji na mashabiki wa Simba, Watanzania sasa tuache tofauti zetu tuunge mkono jitihada za klabu ya Simba wawakilishi wetu ambao kwa hakika wameonesha uwezo mkubwa"
"Bara la Afrika sasa hivi ukizungumza soka lipo wapi watakwambia klabu ya Simba ya Tanzania timu ambayo inatisha sasa Afrika. Zamani ilikuwa DR Congo, Misri, Nigeria lakini sasa hivi Tanzania inaingia"
"Tulikotoka na tunapokwenda klabu ya Simba imenipa raha kwa maana ya kupigania bendera ya nchi kuona inapepea vyema. Wasibweteke na mafanikio ya kuingia Robo Fainali lakini tusiwabeze wanastahili kupongezwa na kuwapa nguvu wajisikie wana wajibu kuhakikisha nchi hii inapata ubingwa wa Afrika," amesema Kifaru