Tuko tayari kuikabili Al Ahly - Manara

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
8 Apr 2021
Tuko tayari kuikabili Al Ahly - Manara

Mkuu wa kitengo cha Habari na Mawasiliano klabu ya Simba Haji Manara amesema wachezaji wote wana ari kubwa kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa barani Afrika dhidi ya Al Ahly amboao utapigwa kesho ijumaa

Simba iliwasili Misri jana na usiku wachezaji wakafanya mazoezi yao ya kwanza nchini humo

Kikosi kitakamilisha mazoezi yake leo tayari kuwavaa mabingwa hao watetzi michuano ya ligi ya mabingwa

Akizungumzia hali ya kikosi, Manara amesema wachezaji wana ari kubwa wakiwa na shauku kupata matokeo hapo Misri

"Wachezaji wote wana ari kuelekea mchezo dhidi ya Al Ahly, ukiwatazama utaona kabisa wana kiu ya kufanya kitu hapa Misri," alisema Manara

"Tayari wachezaji wote wamechukuliwa vipimo vya corona kama CAF walivyoelekeza vipimo hivyo vichukuliwe saa 48 kabla ya mchezo"

"Tunachowaomba mashabiki wa Simba na Watanzania wote huko nyumbani mtuombee dua, sisi huku tumefanya maandalizi ya kutosha, tuko tayari kwa mchezo"

Leo Simba itafanya mazoezi katika uwanja wa Al Salaam ambao utatumika kesho katika mchez huo utakaopigwa kuanzia saa nne usiku

 

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
3h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
9h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
12h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
15h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
16h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
16h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’