Kikosi cha Simba kinatarajiwa kuwasili nchini Misri leo tayari kwa mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Al Ahly utakaopigwa Ijumaa
Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema mchezo wao dhidi ya Al Ahly utakuwa wa kulinda heshima kwani tayari wametinga robo fainali ya michuano hiyo
Akizungumza saa chache kabla ya kuondoka nchini jana, Gomez alisema anataka kuweka heshima dhidi ya mabingwa hao watetezi
"Licha ya kufuzu nataka kuweka heshima ya kutokufungwa katika hatua ya makundi ndio maana nimeondoka na nyota wote," alisema
Simba inaongoza Kundi A ikiwa na pointi 13 ikifuatiwa na Al Ahly yenye pointi nane, AS Vita ina pointi nne na Al Merrikh ina pointi mbili
Simba na Al Ahly zimefuzu hatua ya robo fainali kwa tofauti ya pointi tano
ADVERTISE HERE