Ni faida kubwa kwa Simba kumaliza kinara wa kundi A michuano ya ligi ya mabingwa kwani wamezikwepa timu nyingine tatu zitakazomaliza vinara wa makundi
Timu hizo ni Mamelodi Sundowns, Widad Athletic na Esperance
Lakini pia Simba haiweze kukutana na Al Ahly katika hatua ya robo fainali kwa kuwa timu zote zilikuwa kundi moja
Hizi ndizo timu ambazo Simba itakutana na mojawapo katika mchezo wa robo fainali
KUNDI B - CB Belouizdad / Al Hilal
KUNDI C - Horoya / Kaizer Chiefs
KUNDI D - Zamalek / MC Alger.
Aidha, droo ya hatua ya robo fainali itafanyika April 30 nchini Misri. Simba itaanzia ugenini na baadae kumaliza mchezo wa pili nyumbani
ADVERTISE HERE