Manula atabaki Simba - Gomes

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
5 Apr 2021
Manula atabaki Simba - Gomes

Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema kuwa hakuna ukweli wowote kuhusu tetesi zinazomuhusisha mlinda lango Aishi Manula na klabu ya Al Merrikh inayotajwa kumuwania kipa huyo namba moja kwa klabu ya Simba na timu ya Taifa

Aidha Gomes amesema hashangazwi na tetesi hizo kwani alitarajia kutokana na ubora aliionyesha Manula katika michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu, timu nyingi zitatamani kuwa nae lakini Simba hawatakuwa tayari kumruhusu aondoke

"Hizo taarifa hazina ukweli wowote, mimi nilikuwa kocha wa Merrikh miezi michache iliyopita hivyo nafahamu mikakati yao na niwahakikishie mashabiki wa Simba kuwa Manula atabaki Simba. Kwa sasa yupo kwenye kiwango kizuri na kila timu itahitaji kuwa na kipa kama yeye lakini kwakuwa na Simba ni timu kubwa, basi ataendelea kuwa hapa," alisema Gomes

Manula ameweka rekodi ya kipekee kwenye michuano ya ligi ya mabingwa msimu huu akiruhusu bao moja tu katika michezo minne aliyocheza kwenye hatua ya makundi

Katika kampeni yote ya michuano hiyo, Manula ameruhusu mabao mawili tu

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
4h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’