Baada ya kutinga robo fainali ya michuano ya Ligi ya Mabingwa barani Afrika, Simba imejihakikishia kuondoka na kitita cha Tsh Bilioni 1.5
Mabingwa hao wa nchi sasa wanalenga kuondoka na zawadi kubwa zaidi kama watafanikiwa kutinga nusu fainali
Kulingana na mchanganuo wa zawadi hizo zinazotolewa na (CAF), timu nne zitakazofika nusu fainali zitanyakua kitia cha Th Bilioni 2
Mshindi wa pili ataondoka na Bilioni 2.5 wakati bingwa atanyakua Bilioni 5
Simba ina nafasi kubwa ya kutinga nusu fainali baada ya kumaliza vinara wa kundi A hatua ya makundi
Katika mchezo wa robo fainali wataanzia ugenini kisha kumalizia kwa Mkapa na zaidi watacheza na moja ya timu iliyomaliza katika nafasi ya pili kwenye makundi mengine
ADVERTISE HERE