Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema Wanachama na Mashabiki wa klabu ya Simba ni haki yao kufurahia mafanikio ya timu yao baada ya kufanikiwa kutinga robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika
Gomes amesema Simba sasa ni moja ya timu nane bora barani Afrika, na klabu imeendelea kuimarika
Gomes amewaambia Wanamsimbazi 'wavimbe' na watembee kifua mbele kwani haya ni mafanikio makubwa kwa timu yao
"Kwa sasa ni muda wa kufurahia kufuzu [robo fainali], na pia kufurahia ukuaji wa timu. Simba imekua sana, kwasasa Simba ni moja ya timu nane bora Afrika kwahiyo tufurahie muda huu," amesema Gomes
Simba inasubiri kumalizia mchezo wa kukamilisha ratiba hatua ya makundi kule Misri wiki ijayo na wakati huohuo wakianza kujipanga na mchezo wa robo fainali ambao wataanzia ugenini na kumalizia kwa Mkapa