AS Vita lazima 'wafe' kwa Mkapa

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
2 Apr 2021
AS Vita lazima 'wafe' kwa Mkapa

Mabingwa wa nchi Simba kesho Jumamosi April 03 majira ya saa kumi jioni watashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kusaka matokeo muhimu ambayo yatawapeleka robo fainali ya michuano ya ligi ya mabingwa dhidi ya AS Vita

Simba inahitaji kushinda kwa idadi yoyote na mabao au hata kutoka sare ya aina yoyote kutinga robo fainali

Kwa maana nyingine, Mnyama kesho hapaswi kupoteza mchezo ajihakikishie kwenda robo fainali

Kocha Msaidizi wa Simba Selemani Matola amesema ni lazima washinde mchezo huo ili waweze kutinga robo fainali

Akizungumza na wanahabari mapema leo, Matola alisema wachezaji wote wako katika hali nzuri, maandalizi wamefanya ya kutosha, wako tayari kuwapa furaha Watanzania

"Kesho ni lazima tupate matokeo ili tusonge mbele, tumejipanga kupata matokeo. Tunamshukuru Mungu hakuna mchezaji ambaye tutamkosa, wote wapo kambini na hilo linatupa mwanga kuwa tunaweza kufanya vizuri," alisema

Naye nahodha wa Simba John Bocco amesema uzoefu na maandalizi mazuri waliyofanya ni silaha muhimu kuelekea mchezo wa kesho pale uwanja wa Benjamin Mkapa

"Kwa upande wetu kama wachezaji tuko vizuri, tuna ari nzuri ya kuweza kupambana ili kufikia malengo ya timu yetu. Tumefanya maandalizi mazuri na tunaamini Mungu atatusaidia na tutafuzu hatua ya robo fainali. Tuna wachezaji wenye uzoefu mkubwa na wanaoelewa kwanini wapo kwenye klabu. Tuko tayari," amesema Bocco

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
7h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
13h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
16h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
19h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
19h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
20h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’