Djuma aeleza sababu ya kumtoa Ndemla mapema

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
•
27 Feb 2018
Djuma aeleza sababu ya kumtoa Ndemla mapema
Kocha Msaidizi wa Simba Masudi Djuma ametaja sababu ya kumtoa mapema kiungo Said Ndemla kwenye mchezo dhidi ya Mbao FC ambapo Simba iliibuka na ushindi wa mabao 5-0.

Ndemla alitolewa kwenye dakika ya 30 na nafasi yake kuchukuliwa na Mzamiru Yassini.

Djuma aliwaambia waandishi wa habari baada ya mchezo kuwa waliona haikuwa siku nzuri kwa kiungo huyo kwani hakuwa kwenye kiwango chake cha siku zote.

“Unajua siku hazifanani, huenda leo hakuamka vizuri kwa hiyo huwezi kumkawiza kumtoa kwa sababu siku nyingine huwa anafanya vizuri," alisema Djuma.

"Kama huwa anafanya vizuri, leo hakufanya vizuri, Simba haina mchezaji mmoja, wapo na wengine kama mtu hajaonesha kiwango unampa nafasi mwingine kuliko kuendelea kumwacha wakati game imemkataa.

"Amefanya mistake kidogo hakuwa sawa leo, tukamuingiza mtu mwingine akarekebisha makosa mambo yanaendelea."

Aidha Djuma amepuuza tukio la Ndemla kugoma kumpa mkono kocha huyo baada ya kutolewa.

"Hata mwanamke nyumbani kuna siku mnashindwa kusalimiana na kupeana mkono, hakupi hata kiss hiyo ni mambo ya kawaida kupewa mkono sio lazima lakini kama mchezaji game imemkataa tunamtoa tuna muweka mwingine"

“Wakati Ndemla anatolewa Simba ilikuwa haijafunga goli hata moja lakini baada ya Mzamiru kuingia yakapatikana magoli mawili ya haraka. Mzamiru alitoa assist ya goli la tatu ambalo lilifungwa na Okwi kipindi cha pili."
ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
1m ago
READ MORE →
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE →
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE →
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
20h ago
READ MORE →
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE →
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE →
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE →
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE →
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE →
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE →