Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) limethibitisha kuwa CAF wameiruhusu klabu ya Simba kuingiza mashabiki 10,000 katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya AS Vita utakaopigwa keshokutwa Jumamosi katika uwanja wa Benjamin Mkapa
"Shirikisho la Mpira wa Miguu Afrika (CAF) limeiruhusu timu ya Simba kuingiza washabiki 10,000 katika mechi yao dhidi ya AS Vita kutokana na maombi ya TFF," imebainisha taarifa iliyotolewa na TFF
Sasa ni rasmi 'Mnyama' atawania kutinga robo fainali mbele ya mashabiki wake wazalendo 10,000 ambao wataingia kwa Mkapa!
ADVERTISE HERE