Tutawakabili AS Vita kwa tahadhari - Manula

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
1 Apr 2021
Tutawakabili AS Vita kwa tahadhari - Manula

Mlinda mlango namba moja wa timu ya taifa ya Tanzania na klabu ya Simba, Aishi Manula amesema licha ya klabu yake kuwa vinara wa Kundi A, wataingia kwa tahadhari kubwa katika mchezo ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita kutoka Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo

Simba ikiwa na pointi 10 baada ya kushuka uwanjani mara nne, itakuwa mwenyeji wa AS Vita inayoshika nafasi ya tatu katika mchezo wa tano wa Ligi ya Mabingwa Afrika utakaopigwa keshokutwa Jumamosi kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam.

Manula anaamini kuwa mchezo huo utakuwa mgumu kwa pande zote mbili, kwani lengo lao ni kufuzu na kumaliza katika nafasi ya kwanza wakati wapinzani wao wakitaka kulipa kisasi pamoja na kusaka nafasi ya kufuzu hatua ya robo fainali

"Mchezo wa soka una matokeo matatu kushinda, kushindwa na kutoka sare, mwalimu ametueleza na wachezaji wote tunajua kwamba utakuwa mchezo mgumu kwa sababu kama sisi tuliweza kushinda kwao, hata wao wanaweza kufanya hivyo kwetu kama hatutakuwa makini," alisema

Manula alisema mbali na mbinu walizopewa na kocha mkuu Didier Gomes ambaye amekuwa akisisitiza wachezaji kuongeza umakini ili kuhakikisha wanaondoka na pointi tatu ili kuongeza wigo wa pointi na wale wanaowafuatia.

Alisema wanapaswa kucheza kwa nidhamu ya hali ya juu na kuingia uwanjani kwa kuwaheshimu AS Vita ambao ni moja ya timu ngumu na yenye uzoefu katika Ligi ya Mabingwa Afrika.

Kocha wa Simba, Gomes Da amesema atatumia muda uliobaki kusoma video ya AS Vita katika kipindi hiki kilichobaki kabla ya kukutana na wakali hao wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo Jumamosi

Simba inahitaji sare ya aina yoyote au ushindi ili kutinga hatua ya robo fainali ya michuano hiyo mikubwa kwa klabu Afrika

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
11h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
17h ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
19h ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
23h ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
23h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
23h ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Goals : Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
Kikosi : Simba vs 15 de Agosto, CAFCL R2
1d ago
READ MORE β†’
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
Mnyama kutinga makundi CAFCL kwa rekodi dhidi ya 15 de Agosto leo
1d ago
READ MORE β†’