Tunajiamini, tutawafunga AS Vita - Gomes

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
31 Mar 2021
Tunajiamini, tutawafunga AS Vita - Gomes

Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema maandalizi wanayofanya kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya AS Vita utakaopigwa Jumamosi, yanawapa matumaini ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo

Kikosi cha Simba hakikuwa na mapumziko wakati wa wiki za Kimataifa kwani pamoja na kuwa na idadi ndogo ya wachezaji, waliendelea kufanya mazoezi makali kujiandaa na mchezo huo 

Juzi Jumatatu wachezaji waliokuwa timu ya Tanzania walirejea kikosini wachezaji wengine wakitarajiwa kuanza kuwasili siku ya kesho

Gomes amesema kuwa kikubwa ambacho kinawapa nguvu ya kuamini kwamba watapata matokeo mbele ya AS Vita ni hali ya kujiamini na maandalizi mazuri wanayofanya

Simba inahitaji angalau alama moja tu  kujihakikishia nafasi ya kwenda hatua ya robo fainali, lakini Gomes amesema malengo yao ni kupata ushindi.

"Tuko makini na tumeweka malengo ya kushinda. Tunajiamini, tunao uwezo wa kufanya vizuri na kutinga robo fainali mapema," amesema  Gomes

Mchezo dhidi ya Vita utapigwa Jumamosi April 03 kuanzia saa kumi kamili jioni katika uwanja wa Benjamin Mkapa

Uongozi wa Simba uliomba kwa Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) waruhusiwe kuingiza mashabiki, bado hakuna taarifa rasmi kuhusu ombi hilo

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’