Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes amesema maandalizi wanayofanya kuelekea mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya AS Vita utakaopigwa Jumamosi, yanawapa matumaini ya kufanya vizuri kwenye mchezo huo
Kikosi cha Simba hakikuwa na mapumziko wakati wa wiki za Kimataifa kwani pamoja na kuwa na idadi ndogo ya wachezaji, waliendelea kufanya mazoezi makali kujiandaa na mchezo huo
Juzi Jumatatu wachezaji waliokuwa timu ya Tanzania walirejea kikosini wachezaji wengine wakitarajiwa kuanza kuwasili siku ya kesho
Gomes amesema kuwa kikubwa ambacho kinawapa nguvu ya kuamini kwamba watapata matokeo mbele ya AS Vita ni hali ya kujiamini na maandalizi mazuri wanayofanya
Simba inahitaji angalau alama moja tu kujihakikishia nafasi ya kwenda hatua ya robo fainali, lakini Gomes amesema malengo yao ni kupata ushindi.
"Tuko makini na tumeweka malengo ya kushinda. Tunajiamini, tunao uwezo wa kufanya vizuri na kutinga robo fainali mapema," amesema Gomes
Mchezo dhidi ya Vita utapigwa Jumamosi April 03 kuanzia saa kumi kamili jioni katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Uongozi wa Simba uliomba kwa Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) waruhusiwe kuingiza mashabiki, bado hakuna taarifa rasmi kuhusu ombi hilo