April 03 mabingwa wa nchi Simba watashuka uwanja wa Benjamin Mkapa kuikabili AS Vita katika mchezo wa ligi ya mabingwa
Vinara hao wa kundi A wanahitaji ushindi au hata sare ili kuweza kutinga robo fainali
Hii ni mechi moja kati ya sita ambazo Simba itacheza mwezi April
April 09 Machampioni hawa wa Taifa hili watasafiri nchini Misri kuikabili Al Ahly kisha kurejea jijini Dar es salaam na kuunganisha Bukoba ambako wanakabiliwa na mchezo wa ligi kuu dhidi ya Kagera Sugar April 14
Baada ya mchezo huo, Simba itarejea jijini Dar es salaam ambapo April 18 na 25 watakuwa wenyeji wa Dodoma Jiji na Coastal Union
Mchezo mwingine wa Ligi utapigwa April 28 dhidi ya Mtibwa Sugar, mchezo huu pia ukipigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Aidha ratiba hiyo haijahusisha mchezo wa kombe la FA dhidi ya Kagera Sugar ambao utapangiwa tarehe nyingine baada ya kuingiliana na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya AS Vita, April 03
Simba inaweza kucheza mechi saba katika mwezi wa nne