Lwanga afanyiwa figisu, aikosa Malawi Afcon

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
29 Mar 2021
Lwanga afanyiwa figisu, aikosa Malawi Afcon

Kiungo mahiri wa Simba na timu ya Taifa ya Uganda Taddeo Lwanga leo ameukosa mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu michuano ya Afcon 2021 dhidi ya Malawi baada ya kudaiwa kuwa na virusi vya corona

Mapema kuelekea mchezo huo Chama cha Soka Malawi kiliwazuiwa wachezaji wanne wa Uganda kucheza kwa kisingizio cha kuwa na virusi vya corona

Hata hivyo baada ya Uganda kuweka ngumu, nyota hao walilazimika kufanyiwa tena vipimo na kubainika kuwa hawakuwa na virusi hivyo

Baada ya sintofahamu hiyo wachezaji hao waliruhusiwa kucheza isipokuwa Lwanga

Uganda imepoteza mchezo huo dhidi ya Malawi kwa kufungwa bao 1-0 na hivyo kuondoshwa kwenye michuano ya Afcon wakati Malawi imefuzu kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2010

Baadae Kenya itacheza na Togo ukiwa ni mchezo wa kukamilisha ratiba, Zimbabwe watacheza na Zambia pia ukiwa mchezo wa kukamilisha ratiba

Kesho Msumbiji watacheza na Cape Verde wakati Cameroon wakicheza na Rwanda

Michezo yote hii itahusisha wachezaji wa klabu ya Simba Joash Onyango, Perfect Chikwende, Clatous Chama, Larry Bwalya, Luis Miquissone na Meddie Kagere ambao watakuwa wakiyatumikia Mataifa yao

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’