Gomes amuondoa Lokosa kokosini, atimkia Afrika Kusini

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
29 Mar 2021
Gomes amuondoa Lokosa kokosini, atimkia Afrika Kusini

Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes amevunja ukimya juu ya straika Mnigeria, Junior Lokosa aliyesajiliwa katika dirisha dogo msimu huu, akisema wala hana mpango naye na kama kweli ametimka zake Afrika Kusini kwake ni faraja kubwa na anamtakia kila la heri.

Lokosa alisajiliwa na Simba katika dirisha la usajili wa Shirikisho la Soka (CAF), kuwapa nafasi timu zinazoshiriki michuano yao kuongeza nguvu ili kukabiliana na janga na Corona, lakini tangu atue kikosini hajawahi kutumika kwenye mechi za Ligi ya Mabingwa Afrika.

Mnigeria huyo alisajiliwa kwa mkataba wa miezi sita akiwa mchezaji huru baada kuachana na Esperance ya Tunisia alicheza mechi moja tu ya kirafiki dhidi ya TP Mazembe katika Simba Super Cup na kutumika kwa dakika chache na mazoezini amekuwa adimu kuonekana.

Hata hivyo Kocha Gomea alisema alipata taarifa kwamba mchezaji huyo ametimkia nchini Afrika Kusini.

"Awali nilikuwa sijui lolote kutoka si mchezaji mwenyewe wala kiongozi ambaye alinipa taarifa za Lokosa kwenda Afrika Kusini ili kuwa watu zangu wa karibu wa huko ndio wamenieleza hilo na huenda kuna moja ya timu akajiunga nayo," alisema Mfaransa huyo na kuongeza;

"Kama atakuwa ameamua kuondoka kimya kimya na amepata timu nyingine Afrika Kusini namtakia kila la kheri huko anapokwenda, Lokosa ni mchezaji mzuri ambaye anaweza kukaa na mpira lakini sasa kwa wakati huu Simba inahitaji mchezaji aliye fiti muda wote na jambo lilokosekana kwake"

Juu ya beki Peter Maduhwa aliyesajiliwa pia kwenye dirisha dogo, Gomes alisema ni beki wa kati mzuri lakini kukosa mechi fitinesi kunachangia yeye kukaa benchi.

"Nafurahishwa na ubora ambao Muduhwa anaonyesha mazoezini na hata wenzake wanaelewa hilo lakini kushindwa kucheza katika ligi mara kwa mara hilo ni moja ya shida," alisema Gomes na kuongeza;

"Unajua mabeki wa kati ambao nawatumia mara kwa mara Pascal Wawa na Joash Onyango wanacheza mara kwa mara katika ligi na wamesha elewana inakuwa ngumu na kama nabahatisha kumpa nafasi Muduhwa katika mechi ngumu kama ambazo tunacheza wakati huu."

Alisema anavutiwa naye na naelewa ubora wake ndio maana mpaka sasa bado yupo katika timu yao ya taifa na kuongeza anaangalia namna gani ya kuweza kuwa naye na kumtumia msimu ujao

Credit : Mwanaspoti

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
56m ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
2h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
18h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
FT : Simba 3-0 15 de Agosto, makundi CAFCL kibabe
1d ago
READ MORE β†’