Msemaji na Afisa Habari wa klabu ya Simba Haji Manara amesema kwa sasa mlinda lango Aishi Manula sio wa kuzungumziwa tena hapa ndani jina lake linapaswa lizungumzwe huko nchi za mbali
Kwa mara nyingine leo, Manula ameisaidia timu ya Taifa kuondoka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Libya katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Manula aliokoa michomo ya hatari isiyopungua mitatu ambayo kama sio uimara wake pengine sasa tungekuwa tukizungumza mengine
Manara amempongeza Manula kwa kujiimarisha na sasa amekuwa kipa bora sana mwenye manufaa kwa klabu ya Simba na timu ya Taifa
"Huyu kipa (Manula) kwa sasa yupo katika kiwango bora sana na ndio maana si ajabu klabu kubwa Afrika kumzungumzia"
"Niliwahi kumwambia mara kadhaa wakati ule Simba au Timu ya Taifa ikifungwa, na yeye kuwa 'Bangusilo' wa kulaumiwa, kwamba wewe ni kipa bora mno ila kinachokuponza ni huo muonekano wako tu"
"Kwa sababu makosa yako ni ya kawaida kwa makipa wote duniani. Leo Aishi upo juu na licha ya kudaka sana pia unafanya saves za hatari iwe Kwa Simba au Kwa Stars"
"Kwangu mimi Aishi ndio MVP wangu wa msimu huu so far.. Muhimu kamatia hapo hapo,,soon utaimbwa Afrika nzima"