Tanzania imekamilisha ratiba ya mechi za kuwania kufuzu fainali za Afcon 2021 kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Libya katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa jioni ya leo
Bao pekee la Stars lilipatikana mwishoni mwa kipindi cha kwanza likifungwa na Saimon Msuva kwa kichwa
Tanzania imemaliza katika nafasi ya tatu kundi J ikikusanya alama saba baada ya mechi sita
Tayari ilishaondoshwa katika michuano hiyo baada ya kupoteza mchezo uliopita dhidi ya Guinea ya Ikweta
Stars sasa inaelekeza nguvu zake katika michuano ya kusaka tiketi ya michuano ya kombe la dunia




ADVERTISE HERE