Klabu ya Simba imeliomba Shirikisho la soka Barani Afrika (CAF) wawaruhusu kuingiza mashabiki kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya AS Vita ambao utapigwa April 03 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Huu ni mchezo muhimu ambao Simba inahitaji kushinda au hata matokeo ya sare kuweza kutinga robo fainali
Mchezo dhidi ya Al Merrikh Simba ilipewa ruhusa ya kuingiza mashabiki 200
CAF imeiruhusu Al Merrikh kuingiza mashabiki 1000 katika mchezo wao dhidi ya Al Ahly hivyo yapo matumaini kwa Simba nao kupewa ruhusa hiyo ingawa yawezekana idadi isiwe kubwa
Hata hivyo Simba imejipanga kushinda mchezo huo bila ya kujali uwepo wa mashabiki kama ilivyokuwa mchezo uliopita dhidi ya Al Merrikh
ADVERTISE HERE