Mshambuliaji Junior Lokosa anahukumiwa na nyakati alizotua Simba na sio kuwa ni mchezaji mbaya
Simba ilimsajili Lokosa kwa ajili ya kuongeza nguvu katika kikosi chake kinachoshiriki ligi ya mabingwa
Mfungaji bora huyo wa Ligi Kuu ya Nigeria msimu wa 2018/19, alisajiliwa kwa mkataba wa miezi sita lakini kukiwa na mpango wa kumpa mkataba wa muda mrefu zaidi mwishoni mwa msimu
Hata hivyo ameshindwa kupata nafasi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza kutokana na ubora wa washambuliaji aliowakuta hapo Simba
Chris Mugalu, Meddie Kagere na John Bocco wote wanafanya vizuri na bahati mbaya zaidi Lokosa alisajiliwa kwa ajili ya kucheza mechi sio zaidi ya 11 za michuano ya ligi ya mabingwa
Kocha Mkuu wa Simba Didier Gomes tayari amepata kikosi chake cha kwanza. Sio rahisi kwa kocha kubadili timu yake inayompa matokeo ndio sababu imekuwa ngumu kwa Lokosa kupata nafasi
Lakini pia, mshambuliaji huyo aliyewahi kuitumikia Esperance, amekaa nje mwaka mmoja na zaidi akiuguza majeraha ya goti
Ili kurejea katika ubora wake alihitaji muda wa kucheza lakini kipindi anarejea ndicho kipindi ligi zilisimama kutokana na janga la corona
Lokosa ni mshambuliaji mzuri ambaye anahukumiwa kutokana na nyakati alizotua Simba