Hakuna wa kuizuia Simba isitwae ubingwa msimu huu! Hiyo ndio kauli mbiu ya mashabiki wa Simba leo baada ya kuishuhudia timu yao ikitoa kipigo cha mbwa mwizi kwa Mbao FC katika mchezo wa ligi kuu ya Vodacom mzunguuko wa 19.
Mbao FC imekula mkono! Ndio wamechabangwa mabao 5-0 na Simba iliyo kwenye kiwango bora kabisa msimu huu.
Zahma ya mabao langoni mwa Mbao FC ilianza dakika ya 37 Shiza Kichuya akiitanguliza Simba kwa bao safi.
Dakika nne baadae Emanuel Okwi aliyekuwa nahodha siku ya leo baada ya Bocco kuwa majeruhi, aliiongezea Simba bao la pili kwa mkwaju wa penati kwenye dakika ya 41.

Vijana wa Mbao kwenye kipindi cha pili waliishuhudia Simba ikipiga mpira wa kitabuni na kujikuta wakiruhusu mabao mengine matatu.
Okwi ndiye aliyefunga bao la tatu kwenye dakika ya 69 kabla Erasto Nyoni na Nicholas Gyan hawajafunga kalamu ya mabao.
Okwi ambaye hata hivyo alishindwa kumaliza mchezo huo baada ya kuumia, mabao yake mawili yamemfanya afikishe mabao 16 hivyo kumuacha anayemfuatia (Chirwa) kwa mabao matano.
Ushindi huo pia umeikita Simba kileleni kwa tofauti ya alama nane dhidi ya Yanga ambayo itashuka dimbani keshokutwa kuumana na Ndanda FC.
Simba imefikisha alama 45 wakati Yanga ikiwa na alama 37
Mahesabu ya benchi la ufundi yanaonekana kwenda sawa na hakika msimu huu haitakuwa jambo jepesi kwa timu yoyote kuizuia Simba isitwae ubingwa.
Katika mchezo wa leo Simba iliwakilishwa na;
1. Aishi Manula
2. Shomary Kapombe
3. Asante Kwasi
4. Erasto Nyoni
5. Yusuph Mlipili
6. Jonas Mkude
7. Shiza Kichuya
8. James Kotei
9. Emmanuel Okwi
10. Nicholas Gyan
11. Said Ndemla
Sub
12. Ally Salim
13. Mohamed Hussein
14. Paul Bukaba
15. Mwinyi Kazimoto
16. Mzamiru Yassin
17. Rashid Juma
18. Laudit Mavugo

ADVERTISE HERE