Mwili wa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, awamu ya tano Hayati Dk John Pombe Magufuli hii leo utazikwa katika makaburi ya familia mjini Chato
Maelfu ya Watanzania wanamiminika katika uwanja wa Magufuli ambapo kutakuwa na misa maalumu ya mazishi ya Rais Magufuli ambaye alikuwa kipenzi cha Watanzania
Mapema asubuhi,Β mwili wa Hayati Magufuli ambae alifariki tarehe 17 mwezi Machi kutokana na tatizo la moyo, utapelekwa kanisani kwa ajili ya ibada maalumu
Maelfu ya Watanzania watashiriki maziko hayo huku mamilioni wakitarajiwa kushuhudia tukio hilo mbashara kupitia runinga
Hakika hii ni siku nyingine ngumu kwa Watanzania ambao bado wako katika maombolezo ya kifo chake kilichotokea Machi 17
ADVERTISE HERE