Bao la dakika ya 15 lililofungwa na kiungo mshambuliaji Perfect Chikwende lilitosha kuihakikishia Zimbabwe ushindi muhimu wa bao 1-0 dhidi ya Botswana matokeo ambao yamewahakikishia Zimbabwe kukata tiketi ya fainali za Afcon 2021 zitakazofanyika nchini Cameroon mwakani
Chikwende ameweka kambani bao muhimu ambalo litaingia katika kumbukumbu za Zimbabwe
Aidha Zambia iliungana na Tanzania kuondoshwa katika michuano hiyo baada ya kulazimishwa sare ya mabao 3-3 na mabingwa watetezi Algeria
Kiungo Clatous Chama alikuwa mfungaji wa moja ya mabao ya Zambia
Nyota wengine wa Simba ambao walikuwa uwanjani jana kuzitumikia timu za Taifa ni Joash Onyango (Kenya) akiwa sehemu ya kikosi cha Harambee Stars kilicholazimishwa sare ya bao 1-1 dhidi ya Misri. Kenya pia wameondoshwa katika michuano hiyo
Peter Muduhwa akiitumikia Malawi katika mchezo dhidi ya Sudan Kusini, Malawi wakiibuka na ushindi wa bao 1-0
Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein, Kennedy Juma, Erasto Nyoni, Jonas Mkude, Mazmiru Yassin na Hassan Dilunga walikuwa sehemu ya kikosi cha Stars kilichocheza na Guinea ya Ikweta ambayo ilishinda bao 1-0 nyumbani na kukata tiketi ya kushiriki fainali za michuano ya Afcon 2021