Mfaransa ampa somo Morrison

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
25 Mar 2021
Mfaransa ampa somo Morrison

Kocha Mkuu wa Simba Mfaransa Didier Gomes amesema kuwa kiungo wake mshambuliaji Bernard Morrison ana uwezo mkubwa ila anapaswa aongeze umakini zaidi akiwa uwanjani

Gomes, raia wa Ufaransa amesema kuwa amekuwa akifurahishwa na wachezaji wake wote wakiwa kwenye majukumu yao ila wakati mwingine Morrison amekuwa ni mtu mwenye utani mwingi.

Morrison alikuwa sehemu ya kikosi kilichowavaa Al Merrikh Uwanja wa Mkapa wakati wakishinda mabao 3-0 na kuwafanya waondoke na alama zote tatu huku yeye akitengeneza pasi moja ya bao kwa Mohamed Hussein.

Kiungo huyo alikuwa kwenye ubora wake na alionekana kuwa na maamuzi ya haraka jambo lililomfurahisha Gomes.

"Morrison ni mchezaji mzuri ila kuna wakati mwingine amekuwa ni mtu wa utani, sasa ikiwa timu inahitaji ushindi ni lazima utani uwekwe kando kisha kazi ifanyike.

"Kila mchezaji ndani ya Simba ana uwezo wake na wanategemeana katika kusaka ushindi, bado safari ni ndefu kwani tunahitaji pointi moja ili kufikia malengo ya kutinga hatua ya robo fainali na haitakuwa kazi rahisi ikiwa kutakuwa na utani," amesema.

Aprili 3, Simba itakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya AS Vita mchezo utakaochezwa Uwanja wa Mkapa

GPL

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
5h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
6h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
8h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
12h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’