Chama, Bwalya uwanjani Zambia, kina Bocco wako Guinea ya Ikweta

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
25 Mar 2021
Chama, Bwalya uwanjani Zambia, kina Bocco wako Guinea ya Ikweta

Hii ni wiki ya Kimataifa kwa michuano ya kuwania kufuzu fainali za Afcon 2021 ambayo inafikia tamati mwishoni mwa wiki hii Mataifa mbalimbali yakiwania tiketi ya kushiriki michuano hiyo itakayofanyika nchini Cameroon

Wakati Tanzania ikitarajiwa kushuka uwanjani kule Guinea ya Ikweta kusaka matokeo yatakayowapa tiketi ya kushiriki michuano hiyo, Zambia itakuwa na kibarua kigumu mbele ya mabingwa watetezi Algeria

Viungo mahiri wa Simba Larry Bwalya na Clatous Chama watakuwa na jukumu la kuibeba Zambia katika mchezo huo ambao wanahitaji kushinda

Aidha nahodha John Bocco akiwa sambamba na nyota wengine wa Stars kutoka kikosi cha Simba, Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein, Erasto Nyoni, Kennedy Juma, Mzamiru Yassin, Jonas Mkude na Hassan Dilunga watakuwa na jukumu la kuiwakilisha Tanzania kwa kushirikiana na wachezaji wengine katika mchezo ambao Tanzania haipaswi kufungwa

Nae beki kisiki Joash Onyango leo atakuwa dimbani kuichezea timu yake ya Taifa ya Kenya itakapowakabili Misri katika mchezo utakaopigwa uwanja wa Kasarani

Hapo jana Meddie Kagere alikuwa sehemu ya kikosi cha Rwanda kilichopata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Msumbuji ya Luis Miquissone

Uganda ya Taddeo Lwanga ikalazimishwa suluhu ya bila kufungana dhidi ya Burkina Faso

Mlinzi Peter Muduhwa yeye ataitumikia Zimbabwe itakapowakabili Botswana baadae leo

Ni ishara nzuri kuona klabu ya Simba inatoa wachezaji wengi (18) katika timu za Taifa

Michuano hii inawasaidia wachezaji kujiongezea kujiamini, haishangazi kuona Simba ndio kinara wa kundi A michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
10m ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
1h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
3h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
7h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
19h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
Magazeti ya leo Jumatatu, Oktoba 26 2026
1d ago
READ MORE β†’