Tanzania kibaruani Guinea ya Ikweta

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
25 Mar 2021
Tanzania kibaruani Guinea ya Ikweta

Timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' leo saa nne usiku kwa saa za Tanzania, itashuka Estadio de Malabo kuikabili Guinea ya Ikweta katika mchezo wa kuwania tiketi ya kufuzu fanali za Afcon 2021

Ni mchezo muhimu kwa Tanzania inayosaka nafasi ya kucheza Afcon kwa mara ya pili mfululizo

Tanzania inahitaji ushindi au matokeo ya sare kuelekea mchezo wao wa mwisho dhidi ya Libya ambao utapigwa jijini Dar es salaam Machi 29

Guinea ya Ikweta inashika nafasi ya pili kundi J ikiwa na alama sita wakati Tanzania iko nafasi ya tatu ikiwa na alama nne

Kama Guinea ya Ikweta watashinda leo basi watajihajihakikishia kufuzu Afcon 2021 wakiungana na Tunisia

Lakini matokeo tofauti yanaweza kuipa nafasi Tanzania kutegemeana na matokeo ya mechi za mwisho Tanzania ikicheza na Libya wakati Tunisia watacheza na Guinea ya Ikweta

Jana jioni vijana wa kocha Kim Poulsen walifanya maandalizi yao ya mwisho Estadio de Malabo kuelekea mchezo huo

Nahodha wa Stars Mbwana Samatta amesema kuwa watautumia mchezo huo kumuenzi aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, awamu ya tano Hayati Dk John Magufuli aliyefariki dunia Mach 17

Hayati Magufuli alikuwa na mchango mkubwa katika kampeni za michuano ya Afcon iliyopita. Alitoa fedha za hamasa na kuhakikisha Tanzania inakataba tiketi na ikashiriki fainali hizo za mwaka 2019 ambazo zilifanyika Misri

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
43m ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
3h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
4h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
6h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
10h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
22h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’