Kocha Mkuu wa Simba Queens Mussa Hassan Mgosi amesema wamerejea mazoezi kujiandaa na mechi za lala salama ligi kuu ya Wanawake 'Serengeti Lite' licha ya kuwa kwenye majonzi makubwa kufuatiwa kuondokewa kwa aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Awamu ya Tano, Hayati Dk John Magufuli
Mgosi amesema wanamuenzi hayati Magufuli kwa kutekeleza sera yake ya 'Hapa kazi tu' ndio maana wamepata nguvu ya kurejea mazoezini
"Kwa niaba ya Simba Queens, tunatoa pole kwa Rais Mh Samia Suluhu Hassan na Watanzania wote kufuatia kifo cha aliyekuwa Rais wetu Dk John Magufuli"
"Kwa hakika tumeghubikwa na majonzi makubwa kwa kuondokewa na mpendwa wetu"
"Na licha ya kuwa katika hali hii ya majonzi, tunaendelea kumuenzi kwa sera yake kufanya kazi na kujituma kwa kuendelea na mazoezi ambayo kwa sasa tunafanya mara moja kwa siku," alisema Mgosi
SImba Queens iko kileleni mwa msimamo wa ligi ikiwa imejikusanyia alama 39. Mabingwa hao wa msimu uliopita, wana nafasi kubwa ya kutetea ubingwa wao kwa msimu wa pili mfululizo