Kwa Miquissone ni msimu wa rekodi Afrika

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
24 Mar 2021
Kwa Miquissone ni msimu wa rekodi Afrika

Winga Luis Miquissone amekuwa na msimu mzuri sana aking'ara kwenye kikosi cha Simba katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Akiwa ameweka kambani mabao mawili, Miquissone ametajwa katika kikosi bora cha wiki mara mbili

Aliingia kwa mara ya kwanza baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Al Ahly yeye akiwa mfungaji pekee wa bao hilo

Akafunga tena katika mchezo dhidi ya Al Merrikh na kuingia tena katika kikosi cha wiki

Haya ni mafanikio makubwa kwa Miquissone aliyejiunga na Simba mwishoni mwa mwaka 2019 akitokea klabu ya Mamelodi Sundowns

Katika moja ya mahojiano yake, Miquissone alisema anajisikia fahari kutajwa katika kikosi bora cha wiki mara mbili akieleza kuwa mafanikio hayo ni chachu kwake kufanya bidii zaidi

Alisema yeye na wachezaji wenzake wataendelea kupambana ili kuhakikisha wanafikia malengo ya timu kwani kwake mafanikio binafsi hayawezi kuwa na maana kama hawatafanikiwa kitimu

Miquissone yuko Msumbiji akitimiza majukumu ya timu ya Taifa lakini April 03 atakuwa pale kwa Mkapa katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya As Vita, mchezo ambao Simba inahitaji angalau alama moja kutinga robo fainali

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
3h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
6h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
7h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
9h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
13h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
1d ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’