Nahodha Msaidizi wa timu ya Taifa ya Tanzania 'Taifa Stars' John Bocco amesema Tanzania ina nafasi ya kufuzu fainali za michuano ya Afcon 2021 kama watafanya vizuri katika michezo miwili iliyobaki
Mwaka 2019 Tanzania ilifuzu kwa fainali za michuano hiyo iliyofanyika nchini Misri
Hiyo ilikuwa mara ya pili kwa Tanzania kushiriki michuano hiyo
Stars ikiwa nafasi ya tatu baada ya kujikusanyia alama nne, inaweza kufuzu kama itashinda michezo miwili iliyobaki dhidi ya Guinea ya Ikweta mchezo utakaopigwa ugenini keshokutwa na mchezo dhidi ya Libya utakaopigwa nyumbani Machi 29

Nahodha huyo wa mabingwa wa nchi Simba, amesema kiwango cha soka Tanzania kimepanda na watalidhihirisha hilo kwa kufuzu fainali za Afcon kwa msimu wa pili mfululizo
"Tuna nafasi ya kufuzu tena fainali za Afcon, litakuwa jambo jemba kufuzu kwa mdimu wa pili mfululizo. Tutawadhihirishia wenzetu kuwa kiwango chetu cha soka kimepanda"
"Lakini tunapaswa kupambana uwanjani kuonyesha tunastahili kwenda kushiriki fainali hizo"
"Tumefanya maandalizi mazuri, makocha wameendelea kutuimarisha kimbinu. Kazi itabaki kwetu wachezaji kutumia ujuzi tuliopewa kupata matokeo," alisema Bocco
Stars imeondoka Kenya leo kuelekea Guinea ya Ikweta tayari kwa mchezo huo ambao matokeo yanayohitajika zaidi ni ushindi