Kumekuwa na taarifa kuwa klabu ya Al Merrikh imewasilisha Malalamiko kwa shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF) wakidai kuhujumiwa walipokuja kucheza jijini Dar es salaam na Simba
Ni baada ya wachezaji wao wanane kubainika kuwa na maambukizi ya virusi vya corona na hivyo kuzuiwa kushiriki mchezo huo
Kulingana na nyaraka zilizosambaa kwenye mitandao ya kijamii, Al Merrikh wanadai kuwa waliwafanyia tena vipimo wachezaji hao na kupata majibu kuwa hawakuwa na corona
Majibu hayo yametolewa tarehe 19 Machi, siku tatu baada ya mchezo ambao Simba ilishinda mabao 3-0. Majibu ya kwanza yalifanyika Machi 15 na kutolewa saa chache kabla ya mchezo uliopigwa Machi 16
Inashangaza Al Merrikh kuishushia tuhuma Simba wakati wanaohusika na vipimo vya corona ni Shirikisho la Soka Barani Afrika (CAF)
Walipopimwa, zoezi lote lilikuwa chini ya uangalizi wa CAF hivyo Simba haipaswi kulaumiwa kwa namna yoyote
Lakini pia katika mchezo wa kwanza uliopigwa kwao Sudan, wachezaji watano walizuiwa pia baada ya kubainika kuwa na maambukizi ya corona
Ni katika mchezo huo ambao Merrikh iliwachezesha wachezaji wawili waliokuwa wamefungiwa na chama cha soka Sudan baada ya kusajili katika klabu mbili tafauti
CAF waliwasafisha na kuwaruhusu washiriki mchezo uliopigwa jijini Dar es salaam
Nadhani hawa lengo lao ni kuichafua Simba baada ya kushindwa uwanjani kwani malalamiko yao hayana mashiko
Wanajaribu kulipa kisasi baada ya Simba kuwashitaki wachezaji wao wawili waliokuwa wamefungiwa na CAF
Malalamiko yao hayana mashiko, walipokuja Dar walizidiwa kila kitu. Yani hawa Al Merrikh hata wacheze mechi 10 na Simba hapa Dar watapigwa zote
Kwani ubora wa kikosi cha Simba na wao ni mbingu na ardhi!