Baada ya mapumziko ya siku tatu, kikosi cha Simba kimeanza mazoezi kujiandaa na mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya AS Vita utakaopigwa April 03 katika uwanja wa Benjamin Mkapa
Mchezo huu ndio utaihakikishia Simba tiketi ya kutinga robo fainali kama mabingwa hao wa nchi watapata ushindi au hata matokeo ya sare
Hata hivyo Machampioni hao wa Tanzania wamerejea mazoezini bila ya wachezaji wao 18 ambao wanakabiliwa na makujumu ya timu za Taifa
Akizungumzia kuhusu maandalizi hayo, Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu amesema wameanza mazoezi na wachezaji wachache waliobaki
"Kikosi cha wachezaji wetu ambao hawajaitwa kwenye timu za Taifa wameanza mazoezi ya kujiandaa na mchezo wetu wa tano wa makundi wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita ya DR Congo Jumamosi ya Aprili 3, mwaka huu"
"Tunaweza kuwajumuisha wachezaji wetu wa kikosi cha vijana ili kuhakikisha Mwalimu anakuwa na wachezaji wa kutosha kufanikisha program zake za mazoezi," alisema Rweyemamu