Wachezaji wa klabu ya Simba wamejiunga na kambi ya timu ya Taifa nchini Kenya katika maandalizi ya mechi za kuwania kufuzu fainali za Afcon dhidi ya Guinea ya Ikweta na Libya
Nyota hao walichelewa kujiunga na wenzao kutokana na kukabiliwa na majukumu ya kuiwakilisha Simba katika mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi Al Merrikh uliomalizika kwa Simba kushinda mabao 3-0
Wachezaji hao wamejumuika katika mazoezi ya leo asubuhi na jioni. Aishi Manula, Shomari Kapombe, Mohammed Hussein, Erasto Nyoni, Kennedy Juma, Jonas Mkude, Said Ndemla, Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga na John Bocco wote wamewasili nchini Kenya
Stars inatarajiwa kusafiri kuifuata Guinea ya Ikweta tayari kwa mchezo wa raundi ya tano utakaopigwa Machi 24



ADVERTISE HERE