Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh Samia Suluhu Hassan ametangaza Ratiba ya kuagwa mwili na baadae mazishi ya aliyekuwa Rais wetu Mh Dk John Magufuli aliyefariki dunia juzi kutokana na matatizo ya moyo
Tarehe 20, 2021 Mwili wa Hayati Dkt. John Magufuli utatolewa Hospitali ya Jeshi Lugalo Jijini Dar Es Salaam na kupelekwa katika kanisa la Matakatifu Peter kwa ajili ya ibada na kisha kupelekwa Uwanja wa Uhuru kwa ajili ya kuagwa na viongozi
Tarehe 21, 2021, Wananchi wa Dar Es Salaam wataaga mwili wa Mhe. Dkt. Magufuli katika Uwanja wa Uhuru na baadaye utasafirishwa kwenda makao makuu ya nchi, Jijini Dodoma.
Tarehe 22, 2021 Mwili wa Rais na Amiri Jeshi Mkuu Hayati DKT. Magufuli, utaagwa Jijini Dodoma na kisha kusafarishwa kwenda jijini Mwanza
Tarehe 23, 2021, mwili utaagwa jijini Mwanza na baadaye siku hiyo kusafirishwa kwenda nyumbani kwao Chato, mkoani Geita.
Tarehe 24, 2021 wanafamilia wa Hayati Dkt. Magufuli na Wananchi wa Chato na mikoa ya jirani, watauaga mwili wa mpendwa wetu.
Tarehe 25, 2021 shughuli za mazishi zitafanyika CHATO
Machi 22 na Machi 25, 2021 ni siku za mapumziko