Bado pointi moja tu haooo robo fainali

Mwana Msimbazi By Mwana Msimbazi
β€’
16 Mar 2021
Bado pointi moja tu haooo robo fainali

Wanamsimbazi wana kila sababu ya kufurahi wanapoangalia msimamo wa kundi A michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika

Mnyama yuko juu pale kileleni mbele ya mabingwa wa kihistoria wa bara hili, Al Ahly ambao ni mabingwa watetezi wa michuano hii

Alama 10 baada ya mechi nne, Mnyama amedondosha alama mbili tu huku akiwa hajafungwa hata bao moja, mabao aliyofunga ni matano

Al Ahly wako nafasi ya pili wakiwa na alama zao saba leo wakipata ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya AS Vita kule DR Congo

AS Vita wanashika nafasi ya tatu wakijikusanyia alama nne, wakati Al Merrikh wanaburuza mkia wakiwa na alama moja

Kimahesabu, Simba inahtaji alama moja tu kutoka mechi mbili zilizobaki iweze kujihakikishia kuingia robo fainali

Al Ahly wao wanahitaji alama nne kutoka mechi zao mbili zilizobaki wakati AS Vita watahitaji alama sita

Mechi mbili zilizobaki kwa upande wa Simba ni dhidi ya AS Vita na Al Ahly

Mchezo unaotangulia ni dhidi ya AS Vita wakati mchezo wa mwisho utakuwa dhidi ya Al Ahly kule nchini Misri

Vita watakuja jijini Dar es salaam mwanzoni mwa mwezi April kuikabili Simba katika mchezo ambao lazima Simba apate ushindi au sare kujihakikishia tiketi ya robo fainali

Mchezo dhidi ya Al Ahly kule Misri hautabiriki, hivyo mechi dhidi ya AS Vita hapo kwa Mkapa lazima kieleweke!

ADVERTISE HERE

Simba SC Stories

Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
Janza atangazwa Mkurugenzi wa ufundi Simba
2h ago
READ MORE β†’
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
Barker hamuhofii yeyote makundi CAFCL
4h ago
READ MORE β†’
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
Fountain Gate wanaandaliwa dozi inayowatosha
5h ago
READ MORE β†’
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
Mkutano Mkuu Simba sasa ni Januari 2027
7h ago
READ MORE β†’
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
Magazeti ya leo Jumanne, Oktoba 27 2026
11h ago
READ MORE β†’
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
Mechi dhidi ya Fountain Gate yasogezwa mbele kwa siku moja
23h ago
READ MORE β†’
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
Simba kumuongeza Barker mkataba wa muda mrefu
1d ago
READ MORE β†’
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
Simba yaifuata Fountain Gate Manyara
1d ago
READ MORE β†’
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
Hii hapa miamba 16 makundi CAFCL
1d ago
READ MORE β†’
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
Highlights; Simba 3-0 15 de Agosto, CAFCL (FT)
1d ago
READ MORE β†’