Mabingwa wa nchi Simba wameendeleza rekodi yao ya kibabe katika michuano ya ligi ya mabingwa barani Afrika baada ya kuichapa Al Merrikh mabao 3-0 katika mchezo uliopigwa uwanja wa Benjamin Mkapa
Ndio! hapo kwa Mkapa hatoki mtu,Β itaendelea kubaki hivyo bila kujali kuna mashabiki au la
Wale waliodhani Simba inaweza kuzuiliwa kwa kuwaondolea mashabiki basi ushindi wa leo ni ujumbe wao!
Ulikuwa ni mchezo wa upande mmoja kwa muda mwingi, ubora wa Simba ulitamalaki, mabao matatu yalikuwa machache, Merrikh walistahili kufungwa nyingi



Mpaka wakati wa mapumziko Simba ilikuwa mbele kwa mabao mawili yaliyofungwa na Luis Miquissone na Mohammed Hussein 'Zimbwe Jr' wote wakinufaika na kazi maridhawa iliyofanywa na Bernard Morrison aliyeanza leo
Bao la tatu lilifungwa na Chris Mugalu mapema tu kwenye kipindi cha pili akimalizia kwa shuti kali krosi ya Miquissone
Ni matokeo ambayo yanaifanya Simba kuwa klabu pekee ambayo haijaruhusu hata bao moja kundi A
Wanaendelea kubaki kileleni kwa alama 10, alama moja tu inatosha kuwapeleka wababe hao wa soka hatua ya robo fainali